
UCHAGUZI Mkuu nchini Uingereza unafanyika leo huku mtazamo ukionyesha Chama cha Labour kupewa nafasi kubwa ya ushindi.
Kura za maoni zinaonyesha kwamba Labour ina nafasi nzuri ya kushinda wingi mkubwa kwa kupata kati ya viti 331 hadi 510 kati ya 650.
Chama cha Conservative kwa upande mwingine, kinakabiliwa na kuporomoka kwa kiasi kikubwa, na makadirio yanaonyesha kati ya viti 61 hadi 157.
Waziri Mkuu Rishi Sunak wa Conservative amesisitiza kwamba mfumuko wa bei uko chini ya udhibiti na uchumi unazidi kuimarika, na utabiri wa ukuaji wa 0.5% kwa 2024 na 0.9% kwa 2025.
Kiongozi wa Labour, Keir Starmer, anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuwa Waziri Mkuu ajaye wa Uingereza.