×

#EXCLUSIVE: Bibi Mjane Alia Kuporwa Eneo na Serikali ya Mtaa

Bibi huyu anaitwa Isabela Kigae, Mkazi wa Isakalilo Manispaa na Mkoa wa Iringa.

Bibi Isabella anautuhumu uongozi wa mtaa huo kupanga njama na kuuza eneo lake la ardhi.

Anaeleza kuwa eneo hilo alikuwa akilimiliki tangu mwaka 1946 lakini baada ya mumewe kufariki, hususan mwaka 2020 eneo hilo likaingia katika mgogoro mkubwa, uongozi wa mtaa ukidai eneo hilo ni mali ya serikali na wanahitaji kujenga ofisi ya kijiji.

Kwas asa eneo alilokuwa akilimiliki Bibi Isabella limejengwa ofisi huku mwenyewe akiwa bado katika manung’uniko ya kupambania haki yake.

Global TV imemtafuta Mwenyekiti wa Mtaa wa Isakalilo ambaye amethibitisha ni kweli eneo lilibadilishwa matumizi na kupewa mtu mwingine (mtendaji wa kipindi hicho) na wakakubaliana kujenga ofisi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by globalpublishers (@globaltvonline)

Leave a Comment