
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake, Filipe Nyusi, Rais wa Msumbiji Julai 4, 2024 walitembelea Banda la Vodacom kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba.
Wakiwa kwene banda hilo, marais hao walijionea shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo na kupewa maelezo na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire ambaye aliwaeleza shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Hayo yalifanyika wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya 48 ya Sabasaba ambapo Vodacom pia iliibuka mshindi wa jumla.