Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango leo Januari 20, 2024 amewasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitokea Davos nchini Uswisi.
Dk. Mpango alienda nchini Uswisi kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF).
Katika safari hiyo, Dk. Mpango aliambatana na mkewe, Mbonimpaye
Mpango ambapo wamepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na viongozi wengine mbalimbali.