
Klabu ya Simba imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo ‘mkata umeme’ Yusuph Kagoma kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Singida Fountain Gate.
Taarifa ya Wekundu hao wa Msimbazi inaeleza kuwa “Kagoma ni moja ya Vijana wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuzuia timu ikishambuliwa na kupandisha mashambulizi”