
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Tunduma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Mji Tunduma kuomba nafasi ya kazi iliyotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemuiliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
