
BEKI wa kazi mzawa ndani ya kikosi cha Yanga, Kibwana Shomary ameongeza mkataba mpya utakaomfanya awe na uhakika wa kuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2024/25.
Ni mpaka 2026 nyota huyo aliyeibuka ndani ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro atakuwa hapo kutimiza majukumu yake.
Tayari mabingwa hao wa ligi msimu wa 2023/24 wameanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ukiweka kando Kibwana pia mwamba Farid Mussa naye ni miongoni mwa wachezaji ambao wameongeza mkataba ndani ya kikosi hicho cha Yanga.
Chini ya Miguel Gamondi, Yanga ilitwaa taji la ligi itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa ipo wazi kwamba 2023/24 iligotea hatua ya robo fainali.