
Mzee Bahari Seif Mpendu ni mzaliwa wa eneo la Vijibweni-Kibada jijini Dar es Salaam tangu mwaka 1957 ambaye ametoa kilio chake kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaha kufuatia mgogoro wa eneo lake la zaidi ya ekari 10 mgogoro uliodumu tangu 1970.
Mzee Bahari anasema mgogoro huo ulianza tangu enzi za Hayati Julius K. Nyerere ambapo alikubali kutoa eneo lake hilo kwa wizara ya afya akiahidiwa kulipwa fidia, lakini hadi sasa amekuwa mzee akikabiliwa na maradhi ya kisukari na bado hajapata fidia yoyote.

Mzee Bahari alisema kuwa kuanzia utawala wa Hayati Nyerere kisha Hayati Ali Hassan, Hayati Benjamin Mkapa, Mstaafu Jakaya Kikwete na Hayati John Pombe Magufuli, jambo lake lilikuwa mfupa mgumu hivyo sasa anamuomba Rais Samia pamoja Waziri wa Ardhi Jerry Silaa kuingilia kati jambo hilo ili kupatiwa fidia yake.