×

Tume ya Haki za Binadamu Imeanza Kukusanya Maoni ya Mpango Kazi wa Taifa wa Binadamu na Biashara 

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Nyanda Shuli akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana jukumu la Tume hiyo kutengeneza mpango wa Taifa katika maeneo mbalimbali ya Haki za Binadamu na Biashara.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeanza kutekeleza  jukumu la  kukusanya maoni juu ya mpango kazi wa taifa wa haki za binadamu na biashara .
Jukumu hilo limeanzia kukusanya maoni kwa wenye viwanda na kampuni katika hatua ya kwanza  kumalizika  wanakwenda kwa wafanyakazi ili kuratibu mpango kazi wa Taifa.
Mapema Tume hiyo ilipewa jukumu la kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kuhusiana na namna ya kulinda haki za binadamu na maeneo yaliyopewa kipaumbele ambayo ni pamoja na Nishati, kilimo na uchumi wa buluu,utalii na mengine,katika kulitekeleza hilo tume ilizingatia wajibu wa serikali katika kulinda haki za binadamu kwa kulipa fidia.
 Kamishna wa Tume hiyo, Nyanda Shuli amesema hayo leo Julai 15,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za tawi zilizopo jijini Dar es Salaam.
Amesema Tume ilipewa jukumu la kuratibu mchakato wa uandaji wa mpango kazi wa taifa wa haki za binadamu na biashara jukumu ambalo walipewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili watoe taarifa kwa wananchi ambapo zoezi hilo litawafikia wananchi,wafanyabiashara,sekta binafsi na serikali na tayari mchakato umeanza julai 14 na litaitimishwa julai 22 mwaka huu,”alisema Shuli.
Alisema eneo la haki za binadamu na biashara ni eneo nyeti hivyo serikali imeipa taasisi hiyo dhamana yake ili kulinda haki za binadamu jambo linalohitaji usimamizi na uratibu mzuri.
“Serikali imetuamini kama Tume na tumefanya mchakato huo  na kufanya uchambuzi wa mawazo uliotuongoza kufika hatua nyingine ambayo ni kufanya mapitio ya nyaraka zinazoangalia undani wa haki za binadamu na biashara.
Aliongeza:”maeneo yatakayopewa kipaumbele katika mpango huo ni pamoja na nishati na uzinduaji , uzalishaji, usindikaji , kilimo, uchumi wa buluu, utalii, ukarimu , ujenzi na uchukuzi, huduma za kidigitali, mawasiliano pamoja na biashara na fedha,”amesema.
Aidha Shuli amesema Tume baada ya kuhitimisha uchambuzi huo sasa ni wakati wa hatua ya pili na timu ya wataalamu kutoka kwenye taasisi za serikali , asasi za kiraia na sekta binafsi watakusanya maoni na kuchukua taarifa juu ya  maeneo yaliyoainishwa kama kipaumbele.
“Tutakusanya maoni kupitia hizo timu za wataalamu waliosambaa maeneo mbalimbali nchini na baadhi yetu tutakuwepo kwenye ukanda huu kwa maana ya Dar es Salaam na Pwani tukiwa na lengo la kukutana na wafanyakazi wa kampuni binafsi,lengo ikiwa ni  kukutana na taasisi za serikali na wananchi wanaozunguka maeneo mbalimbali ambayo kampuni za biashara zinafanya kazi kwa kuwapa elimu pamoja na kujua ni fidia kiasi gani wapewe ili kupisha mradi husika kwani ni haki yao ya msingi,” Shuli.
Aliongeza:”baada ya kuhitimisha hatua hiyo  tume itaanda rasimu ya awali ambayo itarejeshwa kwa wananchi ilikujadili kama haki zao zimezingatiwa au la kwani mpango huo umelenga kuweka utaratibu mzuri namna bora ya kulinda haki za binadamu katika biashara,”amesema.

Leave a Comment