×

Jokate Mwegelo Ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi Shule ya Sekondari Msalato

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwegelo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jokate Mwegelo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Msalato ya Jijini Dodoma ambayo ni miongoni mwa Shule kongwe za Wasichana zenye historia ya kutoa Viongozi wengi Nchini.

Jokate amefika Shuleni hapo Julai 18,2024 na kuongea na Walimu ikiwa ni wiki moja tangu ateuliwe na Wajumbe wa Bodi ambapo amewaomba Walimu na Watumishi wa Shule hiyo kujituma ili kuhakikisha wanaendeleza historia nzuri ya Shule hiyo.

Jokate amesema “Nimewambia Walimu nina kahistoria na Shule hii ya Msalato kwa maana Mama yangu alisoma hapa hata Mimi nilivyomaliza kidato cha nne kuingia kidato cha tano nilichaguliwa form five PCB kuja kusoma hapa ingawaje sikuja na nilibadilisha mchepuo (combination), kwahiyo najisikia fahari kuwa sehemu ya Jumuiya ya Shule ya Msalato na ukitaja Msalato Nchi nzima wanajua ni Shule ya kitaifa na ina historia njema na imekuwa ikitoa Wasichana vinara kitaaluma na kwa kushirikiana na Bodi yetu mpya tutashirikiana na wenzetu hawa kuendeleza mazuri”

Jokate amesema Bodi kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali watahakikisha wanaboresha miundombinu ya Shule hiyo ikiwemo kupandisha ukuta wa Shule na upatikanaji wa maji safi na salama.

INJINIA HERSI AFUNGUKA MAZITO AWAPA ONYO WAZEE wa YANGA / MAGOMA AMJIBU HERSI /DILI la AWESU

Leave a Comment