Mbunge wa Jimbo la Sengerema Hamis Tabasamu amefanya ziara Jula 19, 2024 katika Kijiji cha Isole Kata ya Buyagu ya kusilikiza na kutatua kero za wananchi.

Mojawapo ya miradi inayoenda kukamilishwa ni pamoja na mradi wa umwagiliaji ambapo zaidi ya watu 2000 wanatarajia kunufaika na miradi ya umwagilijia inayotekelezwa kwenye Kata ya Katunguru na Buzilasoga zilizopo Halmashauri ya Sengerema, ambapo takribani ya kiasi cha Shilingi Bilioni 39.4 zitatumika kufanikisha miradi hiyo.
Tabasamu amewatoa hofu wananchi wa Sengerema wanaopitiwa na miradi hiyo kuwa Serikali haitawanyang’anya mashamba yao watabaki wanayamiliki na kupewa hati ya umiliki wa mashamba yao, ameendelea kueleza kuwa sehemu yoyote linapotokea suala la maendeleo lazima kutatokea misuguano hivyo wasifuate masuala ya watu wapotoshaji wanaokwamisha maendeleo ya wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Isole wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwaletea Kilimo cha umwagilijia ambacho kitawasadia kuwapata chakula Cha kutosha na kuendesha maisha yao.
Mhandisi wa Kilimo Halmashauri ya Sengerema Samson Misambo amesema kuwa miradi hii itakapokamilika itakuwa na manufaa makubwa kwa jamii, manufaa hayo ni kuongeza uzalishaji wakulima watalima zaidi ya mara mbili hii itaongeza viwanda vya kuchekecha zao la mpunga.