Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amewaambia Maafisa Usafirishaji wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kinawapenda na kuwathamini sana maafisa Usafirishaji kwani ni injini muhimu katika ukuaji wa uchumi katika Taifa letu.

Ndugu Jokate ameyasema hayo alipokua anazungumza na Maafisa Usafirishaji (Madera wa Boda boda) Mkoa wa Dar es Salaam kwenye zoezi la uzinduzi wa Usajili wa Wanachama Kieletroniki kwa Maafisa hao wa Usafirishaji.

“Ndugu zangu Chama Cha Mapinduzi kinawapenda na kuwathamini sana Vijana, ninyi ni watu muhimu katika shughuli zetu za kila siku, ninyi ni mashahidi kulikua na kero kibao hata kuingia mjini ilikua ngumu, lakini Chama Cha Mapinduzi kwa kushirikiana na Serikali tumeweza kuondoa vikwazo vyote sasa mnafanya kazi zenu bila bughudha yoyote”