
Mamlaka ya Afya ya mimea na viuatilifuy Tanzania (TPHPA) imesema Mamlaka hiyo imejipanga kutumia maonyesho yanayoendelea kwenye maonyesho ya sikukuu ya wakulima nanenane kanda kutoa elimu ya Afya ya mimea kwa wananchi.
Elimu hiyo itatolewa kwenye viwanja vya Nyam’hongolo Mkoani Mwanza ambapo wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kupatiwa elimu na njia sahihi za udhibiti wa viuatilifu.
Kwa Mjibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Prof. Joseph Ndunguru amesema wameboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi na hivyo wakulima wote nchini watanufaika na huduma zinazotolewa na TPHPA.
Aidha Prof. Ndunguru amebainisha kuwa TPHPA kwa sasa wanazo ofisi katika mipaka yote ya nchi ,viwanja vya ndege pamoja na Bandari yote ikiwa ni mkakati wa kuwafikia wananchi .

