
Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi tukio la Ukatili linaloonekana katika Video inayosambazwa Mitandaoni ikimwonesha Mwanamke anayedaiwa kutokea Yombo Dovya akidhalilishwa
Pia, Jeshi la Polisi limeomba watu wenye taarifa zinazoweza kusaidia kuwapata wahusika wa tukio hilo, wazifikishe kwa Kiongozi yeyote wanayemwamini au waripoti kupitia namba za Simu 0699 998 899Aidha, kupitia Mtandao wa X (zamani Twitter), Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amehimiza pia watu kutoa ushirikiano wa taarifa kwa Jeshi la Polisi

