
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS, akichukua nafasi ya Casmir Kyuki aliyemaliza muda wake
Aidha, Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP), huku Prof. Ahmed Mohamed akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa kipindi cha Pili
