×

Bodi Ya Nyama Yawataka Wafanya Biashara Wa Nyama Kutumia Zana Za Kisasa Kulinda Afya Ya Walaji

 
Bodi ya Nyama Kanda ya kaskazini imeendelea kutoa elimu na kuonyesha vifaa sahihi ambavyo vinatakiwa kutumika na maduka ya nyama huku likiweka wazi kuwa mbali na kutoa elimu hiyo imekuwa ikichukua hatua za kisheria kwa baadhi ya wafanyabiashara wa zao hilo wnaokiuka sheria.
Akitoa maelekezo hayo leo Agosti 7,2024 katika Banda ya wizara ya Mifugo na Uvuvi lilipo katika viwanja vya nane nane Njiro Jijini Arusha Patrick Kaaya ambaye ni afisa mfawidhi bodi ya nyama kanda ya kaskazini amesema wanaendelea kuonyesha na kutoa elimu kwa wafanya biashara wa zao la nyama,wananchi namna sahihi na matumizi ya vifaa vya kisasa ili kumlinda mlaji Wanyama.
Bwana Patrick ameongeza kuwa bodi ya nyama kanda ya kaskazini inafuata sheria zilizoundwa kwa ajili ya kusimamia biashara hiyo ambayo inasimamiwa na sheria ya tasnia ya nyama namba kumi 2006 ili kuweka mazingira salama kwa walaji.
Aidha amesisitiza kuwa bodi hiyo imekuwa iendelea kuchukua hatua kwa watu wanaokiuka sheria na taratibu na miongozo ya bodi ya nyama ili kuweka mazingira bora ya walaji Wanyama ambapo amewataka wafanya biashara hao kufuata taratibu zilizopo.
Na Mwandishi wetu, Arusha.

AMOS wa TEGETA AKAMATWA kwa TUHUMA za KUSAMBAZA TAARIFA za BINTI wa YOMBO KUFARIKI WAKATI YUPO HAI

Leave a Comment