×

Rais wa Comoro Azali Assoumani amempa Mamlaka ya Urais mwanawe, Nour El Fath

Rais wa Comoro Azali Assoumani

Rais wa Comoro Azali Assoumani amempa Mamlaka ya Urais mwanawe, Nour El Fath na kumruhusu kuingilia kati katika hatua zote za maamuzi ya serikali baada ya kumweka msimamizi wa kuratibu masuala ya Serikali mwezi uliopita.

Assoumani, 65, ambaye kuchaguliwa kwake tena Januari kulikumbwa na madai ya udanganyifu wa wapiga kura, ameshutumiwa na wapinzani katika taifa hilo la Bahari ya Hindi kwa kumwandaa mwanawe kuchukua nafasi yake wakati muhula wake utakapokamilika 2029.

Katika jukumu lake, Mamlaka ya El Fath yatajumuisha kutathmini Mawaziri na kuingilia kati katika hatua zote za utekelezaji wa maamuzi ya serikali, kulingana na amri ya Rais iliyochapishwa Jumanne.

Nour El Fath

Msemaji wa serikali Fatima Hamada alisema agizo la Rais lilifafanua na kurasimisha mamlaka ya El Fath kama Katibu Mkuu.

Comoro imeshuhudia takriban Mapinduzi 20 au majaribio ya mapinduzi tangu ilipojinyakulia Uhuru kutoka kwa Ufaransa mwaka 1975.

Assoumani aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 1999 kupitia mapinduzi na ameshinda chaguzi nne tangu 2002.

Leave a Comment