×

Rais Samia Awataka Wananchi wa Tabora Kulinda Miundombinu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi mkoani Tabora

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani mkoani Tabora amewaasa wananchi wa mkoa huo kuilinda miundombinu ambayo imejengwa na Serikali.

 

Akiongea na wananchi katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Rais Samia amesema:

 

“Wana Tabora popote mlipo kulinda miundombinu tunayoinjenga, miundombinu hii ni ya gharama sana kwahiyo naomba sana tunapojenga miundombinu ninyi muwe walinzi wa miundombinu yenu.”

 

Akiongea mbele ya halaiki Rais Samia amegusia suala la ajira kwa kutoa rai kwa wananchi wa Tabora kuchangamkia fursa mbalimbali za kuajiriwa pamoja na kujiajiri kupitia shughuli za ujenzi wa miundombinu hiyo.

Umati wa wananchi waliokuwa wakimsikiliza Rais Samia katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi

Rais Samia amewahimiza Mawaziri kutoka Wizara mbalimbali waliongozana naye katika ziara hiyo akiwemo Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri Bashe, Waziri Makame Mbarawa, Waziri Aweso pamoja na Waziri Bashungwa.

 

 

 

Leave a Comment