
Msanii wa Bongo Muvi, @bintsuzy amefunguka kuhusu tatizo lake la kupenda kula nyama mbichi na kudai kuwa tangu aanze kula hajawahi kupata tatizo lolote la kiafya kama kuumwa tumbo wala minyoo na kwamba hawezi kuacha kwani anapenda mno kula nyama mbichi.
Akizungumza na Global Tv, Suzy anasema kuwa hakuna hata siku moja nyumbani kwake hakuna nyama mbichi kwenye friji, hivyo watu wasimuogope kabisa kwani ni binadamu wa kawaida.