×

Rais Samia Amteua Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Atenguliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ambapo kwa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Mhe. Jenista Joackim Mhagama kuwa Waziri wa Afya.

Mhagama ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) anachukua nafasi ya Ummy Mwalimu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Leave a Comment