×

Wabunge Chama Tawala Wazichapa na Wapinzani Kavukavu Bungeni Nchini Uturuki,

Vurugu kubwa zimeibuka kwenye Bunge la Uturuki kufuatia mjadala mkali uliosababisha mbunge wa upinzani kuwaita chama tawala kuwa ni magaidi.

Patashika hilo lililosababisha wabunge kuzichapa kavukavu, liliibuka bungeni Ijumaa ya Agosti 16, 2024 wakati wa mjadala juu ya kufungwa jela kwa kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo aitwaye Can Atalay.

Mbunge Ahmet Sik wa Chama cha Workers’ Party of Turkey, akiwa katikati ya hotuba yake akitaka Atalay kuachiwa huru ndipo mbunge mwingine Alpay Ozalan wa chama tawala cha AK akamrukia na kumpiga kofi.Kwa haraka, dazeni ya wabunge wakajiunga kwenye kuzichapa kiasi cha kuonekana damu zikiruka na kuonekana kwa waliovalia nguo au mashati meupe.

Atalay ambaye alikuwa tishio kwenye uchaguzi wa mapema mwaka huu nchini humo amefungwa jela miaka 18 baada ya kukutwa na hatia ya kutaka kupindua serikali ya Uturuki.

Leave a Comment