
MBUNGE wa Jimbo la Mtera, Livigstone Lusinde, amempongeza Rais Magufuli, kwa juhudi kubwa anazozifanya za kuiletea nchi maendeleo, ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kufufua shirika la ndege nchini na kuileta ndege ya Bombadier na kuzindua mradi mkubwa wa kufua umeme.
Mbunge Lusinde amejibu hoja ya Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, aliposema kuwa ni aibu kuona Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, anatokea Kusini lakini eneo hilo lina sua sua kwenye miradi wa gesi, ambapo Lusinde amemjibu na kusema Waziri Mkuu sio wa Kusini bali ni waziri wa Tanzania nzima hivyo haipaswi kumgawa kwa kigezo hicho.
Wakati Mbunge Lusinde akichania hoja, Mbunge wa Geita Mjini alimuomba Spika ampe nafasi ya kutoa taarifa katika hoja hiyo.