×

Mbunge Ummy Mwalimu Amshukuru Rais Dkt. Samia kwa Kumwamini

Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu.

Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya Uwaziri wa afya, huku akisema, amepokea mabadiliko yaliyotokea kwa moyo mkunjufu.

Mbunge huyo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa ya moyoni mbele ya Mlezi wa Chama hicho tawala Mkoani Tanga ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleima Abdulla aliye katika ziara ya siku nne Mkoani hamo.

Mlezi wa Chama hicho tawala Mkoani Tanga ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hemed Suleima Abdulla

Katika mazungumzo yake hayo, Ummy Mwalimu alisema, anamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kukwamini kuwa Waziri kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu akianza kama Waziri ofisi ya Rais Tamisemi na baadaye kuwa Waziri wa afya.

“Mheshimiwa mgeni rasmi, naomba umfikishie Salaam za upendo Mheshimiwa Rais, kwa kuheshimu aliyonipatia ambayo pia ilikuwa heshima kubwa kwa watu wa Tanga mjini” alisema Mbunge Ummy Mwalimu.

Aidha alisema kwamba, mabadiliko yaliyotokea ameyapokea kwa moyo mkunjufu na Shukrani ” Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yaliyotokea na kubwa nitaendelea kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Viongozi na chama”.

Ummy Mwalimu aliendelea kueleza kuwa kazi iliyopo mbele yake ni kufanya kazi kwa karibu na wananchi ambao wamemchagua na kumpa heshima ya ubunge akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhfa huo Jimbo la Tanga.

Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa kazi kubwa iliyopo mbele ni kuendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM huku akimpongeza Mwenyekiti wa chama hicho tawala wilayani Tanga Meja mstaafu Hamisi Mkobo akimweleza kuwa Kiongozi asiye na.makandokando.

Ameendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji Ilani kwa mwaka 2020 / 2025 huku akisema vikao vitafanyika kuleleza yaliyotekelezwa.

Amesema, watu wa Tanga wana kila sababu ya kusimama kifua mbele kwa jinsi ambavyo Rais Dkt Samia ameweza kuwabeba katika suala la uboreshaji wa Bandari ya Tanga ambapo Shilingi Bilioni 429 ziliwekezwa na Serikali.

“Niliwaambia watu wa Tanga nataka Tanga iwe kama Singapore maana yake Meli kubwa zitie nanga na kazi imeanza.Tuna deni kubwa kwa Rais Samia yeye hatumdai ila anatudai ushindi wa kishindo sababu meli kubwa zinatia nanga” alisema Ummy.

RAIS MWINYI AZINDUA KIZIMKAZI FESTIVAL 2024 – MAFATAKI YAPIGWA ZANZIBAR – ATOA MAAGIZO….

Leave a Comment