
Mapema leo Agosti 26, 2024 waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefika makao makuu ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Ubungo Dar Es salaam (DAWASA) kwa lengo la kuzindua kampeni mahususi ya DAWASA Mtaa kwa Mtaa.

Lengo la Kampeni hii ni kuongeza uelewa wa utoaji wa huduma za Maji, kusikiliza Maoni na changamoto za kihuduma na pia kuwafikia Wananchi na wateja wengi.

Aidha, Waziri amefanya na kikao kazi na Wazabuni, Wakandarasi na watoa huduma kwa DAWASA kwa lengo la kusikiliza ushauri, changamoto kwa lengo la kudumisha msingi imara wa mahusiano na mashirikiano.


