



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameutana na kufanya mazungumzo.nq Waziri wa Idara ya Mamabo ya Nje wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndugu Liu Jianchao ambaye amesema kuwa CPC na serikali yake, wanatambua Juhudi za kuleta maendeleo zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndugu Jiancho amesema kuwa chini ya uongozi wa Mhe. Samia, Tanzania imekuwa na mabadiliko makubwa, yanayoonekana katika nyanja zote za viashiria vya ukuaji uchumi.