×

Mamia Wampokea Hapi Wilayani Makete Mkoani Njombe

Wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM katika kata ya Iwawa Wilayani Makete Mkoani Njombe wamejitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Jumuiya ya CCM Ndg Ally Hapi ambaye amewasili wilayani humo ikiwa ni katika mwendelezo wa ziara yake mkoani humo

Ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa yenye lengo la kuijenga jumuiya na chama cha mapinduzi pamoja na kueleza kazi iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita ilianza Agost 26 mwaka huu katika wilaya ya Njombe na sasa inaendelea katika wilaya ya Makete

Baada ya kuwasili katika wilaya hiyo Hapi amepokea taarifa ya uhai wa Jumuiya hiyo ya wazazi ikiwa ni pamoja na shughuli za uandikishaji wanachama wapya kupitia mfumo wa Kidigitali ambapo chama cha mapinduzi kinatekeleza zoezi hilo kote nchini.


Hapi, licha ya kuwapongeza jitihada hizo zinazofanywa na viongozi wa chama na jumuiya zake lakini ameeleza namna wanavyopaswa kuendelea kusimamia maono ya mwenyekiti wa chama Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama katika miradi mbalimbali.

“Kama mnavyofahamu Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa Dk.Samia Suluhu Hassan halali usingizi akiwaza kuwaletea wananchi maendeleo hivyo ni wajibu wetu kama viongozi wa chama kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama cha mapinduzi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu”alisema Hapi
Katika Hatua nyingine Hapi alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanaccm kujiandaa na shughuli ya uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 nmwaka huu huku akiwataka kuendelea kuhimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uboreshaji wa taarifa zao katika daftari la makazi ili wawe na haki ya kushiriki katika uchaguzi huo.

Kwa upande wao viongozi wa Jumuiya hiyo katika wilaya yan Makete wamemhakikishia katibu Mkuu juu ya ushindi wa chama cha mapinduzi katika chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka ujao ambapo wanasema watasimama na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan

RAIS SAMIA YUPO ARUSHA KWA MAKONDA – AKISHIRIKI UFUNGUZI WA KIKAO KAZI CHA WENYEVITI WA BODI

Leave a Comment