
Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson amekemea kauli za baadhi ya watu za kuvihusisha vyombo vya dola na matukio ya uvunjifu wa amani yanayotokea katika jamii.
Dkt. Tulia ametoa kauli bungeni Jijini Dodoma baada ya Mbunge wa viti maalum, Anatropia Lwehikila kumuuluza swali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri MKuu kuhusu mkakati wa Serikali wa kuzuia matukio ya utekaji na kupotea kwa watu ambayo alidai yanahusishwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imeendelea kusimamia misingi ya haki na amani kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi ili wananchi na mali zao wawe salama huku akitoa wito kwa jamii kutoa taarifa za uvunjifu wa amani kwa vyombo vya usalama ili hatua stahiki zichukuliwe na si kupotosha jamii kwa kuhusisha vyombo hivyo na matukio ya kihalifu.