
MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Leonel Ateba anatarajiwa kuanza kazi rasmi leo Agosti 31, 2024 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Ingizo hilo jipya limekuja kuchukua nafasi ya Michael Fred, maarufu kama fungafunga ambaye amekutana na Thank You Simba huku rekodi zikionyesha kuwa alifunga mabao sita ndani ya ligi msimu wa 2023/24.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kila kitu kuhusu mchezaji huyo kimekamilika na sasa ruksa kwake kucheza katika mechi za ushindani ataanza na Al Hilal.
“Mfungaji Ateba tayari taratibu za vibali vyake zimekamilika kilichobaki ni Wanasimba kumuona uwanjani akifanya kazi yake ataanza na mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Al Hilal ya Sudan maarufu kama timu ya Ibenge.”
Stori na Lunyamadizo Mlyuka | GPL