×

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Yatoa tahadhari kutokea kwa Upepo Mkali

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa, kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumapili Septemba 1 hadi 3, 2024 katika baadhi ya mikoa nchini.

Upepo huo unatarajiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa kusini mwa Ziwa Tanganyika ikiwemo mikoa ya Rukwa na Katavi na kugusa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Kaskazini mwa bahari ya Hindi ikiwemo mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na kujumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

RC MAKONDA ATEMA NYONGO MBELE ya RAIS SAMIA – AMTANIA SIMBACHAWENE – UKUMBI MZIMA WACHEKA…

Leave a Comment