×

BRELA Yashauriana na Wadau Kuhusu Mkataba wa Sheria ya Kimataifa ya WIPO

Bw. Mustafa Haji ambaye Msajilii Msaidizi (BPRA).

Dar-es-Salaam, 5 Septemba 2024: Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imefanya  kikao cha mashauriano na wadau kuhusu mkataba wa sheria ya kimataifa ya (WIPO) inayihusu ulinzi wa maumbo na michoro ya miliki ubunifu.

Akizungumza na wanahabari, jana, Bw. Godfrey Nyaisa ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) amesema Tanzania ni moja ya nchi wanachama wa shirika la miliki ubunifu duniani (WIPO) na shirika la miliki ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO) kupitia mashirika haya  Tanzania imesaini na kuridhia mikataba na itifaki mbalimbali zinazohusu usimamizi na uratibu wa miliki ubunifu kikanda na masuala mengine.

Bw. Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)

“Mikataba na itifaki hizi zimewekwa mifumo katika kuhakikisha usimamizi na uratibu thabiti wa miliki ubunifu kimataifa ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani hasa katika nyanja ya teknolojia na ubunifu. Nchi wanachama wa WIPO zimeendelea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu inatumika kama chachu ya maendeleo duniani hii imefanyika kwa kufanya majadiliano kwa kukabiliana kuanzisha mikataba katika maeneo muhimu ya umiliki ubunifu.

“Kwa sasa kuna ushindani mkubwa wa kibiashara nchini na nje ya mipaka ya nchi hasa katika kuongeza ubora wa biashara au huduma na muonekano unaovutia wa bidhaa hivyo tunatakiwa kuhakikisha bidhaa zetu ikiwemo vifungashio na mikebe zinakuwa na ubunifu wa kipekee. tunatakiwa kuhakikisha bidhaa au huduma ina muonekano unaovutia.” Amesema Bw. Nyaisa.

Wadau wakisikiliza kiumakini.

Pia ameongeza kuwa watakwenda kufanya mafunzo kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo vijana wadogo ili mtoto awe na uelewa kuhusu ubunifu.

Bw. Mustafa Haji ambaye Msajilii Msaidizi (BPRA) ambaye amumuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji BPRA Bw. Khamis Juma amesema kuwa sekta nzima inayohusiana na miliki ubunifu Tanzania Bara na Zanzibar inafanya kazi zake katika kuhakikisha inashirikiana na mamlaka husika ili kuweza kupiga hatua za maendeleo na uchumi kwa ujumla.

Picha ya pamoja baada ya mkutano huo.

“Tumekuwa tukifanya kazi kwa pamoja katika kutoa elimu kushirikiana katika mikataba mbalimbali ya kimataifa na kitaifa kuhakikisha kwamba Tanzania inachukua kuona miliki ubunifu inafanikiwa kwa kiasi kikubwa.” Alimaliza kusema Haji.

Leave a Comment