
KUELEKEA mchezo wa marudiano dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa leo Jumamosi, kocha Mkuu wa kikosi cha klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa amelazimika kutazama tena mara mbili rekodi ya mchezo uliopita ambayo ni sawa na dakika 180, ili kujua nini wanatakiwa kufanya ili kupindua matokeo yao ya kwanza.