
Jeshi la Polisi Wilaya Tanga wamezuia mkutano hadhara uliotarajiwa kufanyika leo 20/09/2024 Tanga Mjini, mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti Bara Tundu Lissu kwa kile walichodai kuwa mkutano huo ni maandalizi ya maandamano ya Septemba 23, 2024 Jijini Dar es salaam.
Mkutano huo ulikuwa uambatane na zoezi la kuhani msiba wa Mzee Ali Mohamed Kibao.

