
Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara imeendelea Septemba 20, 2024 ambapo katika mchezo wa mapema Fountain Gate Fc imeendeleza mwenendo mzuri baada ya kuibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji Tabora United katika dimba la Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Huu ni ushindi wa tatu kwa Fountain Gate Fc kwenye mechi tano za mwanzo wa msimu sare moja na kipigo kimoja huku wakikwea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi alama 10 baada ya mechi 5. Tabora United wanasalia nafasi ya 5 alama 7 baada ya mechi tano.
FT: Tabora United 1-3 Fountain Gate
⚽ Yacouba Dogne 77’
⚽ Kihimbwa (P) 27’
⚽ Edgar William 37’
⚽ Edgar William 90’
Edgar Williams amehusika kwenye mabao yote ya Fountain Gate Fc akisababisha penalti iliyowekwa kambani na Salumu kihimbwa kabla ya yeye mwenyewe kuingia kambani mara mbili.