×

Kitawaka leo Azam dhidi ya Simba Zanzibar, Kagoma na Mzamiru ‘OUT’

KITAWAKA leo katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Azam dhidi ya Simba Mchezo huo utakaosimamiwa na Mwamuzi Hery Sasii utachezwa saa 2:30 usiku utakuwa wa tano kwa Azam wenye pointi 8 baada ya mechi nne huku ukiwa mchezo wa tatu kwa Simba wenye alama 6.

Simba itakosa nyota wake wawili Yusuph Kagoma na Mzamiru Yassin kukotana na majeraha huku Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally akisema kukosekana kwa nyota hao ni pengo lakini wana timu kubwa na ina wachezaji wengi.

Azam imepoteza mara mbili mfululizo kwenye mechi zilizopita dhidi ya Mnyama wakipoteza 3-0 kwenye Ligi mnamo Mei 9, 2024 kwa magoli ya Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma na David Kameta ‘Duchu’ baada ya kupoteza 1-0 kwenye fainali ya kombe la Muungano 2024 kwa bao pekee la Babacar Sarr.

MUTALE – “SIMUOGOPI MCHEZAJI YEYOTE – CHE MALONE NDIYE MCHEZAJI MWENYE NGUVU KWENYE TIMU”…

Leave a Comment