×

CRDB Kuwekeza Dola Milioni 320 Kwa Wajasiriamali Wanawake na Vijana

Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano wa uwezeshaji wa Dola za Marekani Milioni 320 na Shirika la Kimataifa la Ufadhili wa Maendeleo la Marekani (DFC) na Citibank ili kusaidia zaidi ya wajasiriamali wadogo 4,500 nchini Tanzania na Burundi.

Mkataba huo wa makubabaliano ulisainiwa kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) Makao Makuu ya Citibank katika Jiji la New York, na kushuhudiwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassima Majaliwa, ambapo aliambatana na Waziri wa Uwekezaji na Mipango, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Balozi wa Tanzania Marekani, Mhe. Balozi Elsie Kanza, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Seikali yetu, na Serikali ya Burundi.

Makubaliano hayo ambayo Benki ya CRDB imeingia na DFC, na Citibank yanalenga kuwezesha biashara ndogo na za kati zinazoongozwa na wanawake na vijana, kwa kuwapatia uwezeshaji wa kifedha unaohitajika ili kukua na kustawi kwa biashara zao.

Katika makubaliano hayo, Dola za Marekani Milioni 60 zimetengwa mahsusi kwa ajili ya ufadhili wa biashara zinazomilikiwa na wanawake nchini kupitia programu ya DFC ya uwezeshaji wanawake ya 2X, pamoja na program zinazotekelezwa na Benki yetu za CRDB Malkia, IMBEJU kupitia CRDB Bank Foundation. Uwezeshaji huu ni sehemu ya jitihada za Kuchochea usawa wa kijinsia, na kuwezesha wajasiriamali wanawake kustawi, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

 

Leave a Comment