×

Kesi ya Kumuondoa Gachagua Madarakani Yatua Bunge la Seneti

Naibu wa rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

BUNGE la Seneti nchini Kenya litaanza kujadili hoja ya kumuondoa ofisini Naibu wa rais, Rigathi Gachagua siku ya Jumatano na Alhamisi wiki ijayo.

Seneti leo Oktoba 9, 2024 imefanya kikao kupokea hoja hiyo kutoka kwa Kiongozi wa walio wengi Aaron Cheruyot baada ya bunge la kitaifa kupiga kura ya kumuondoa ofisini Gachagua siku ya Jumanne Oktoba 8, 2024.

Bunge la Seneti litachunguza mashtaka dhidi ya Gachagua na kusikiliza ushahidi kutoka pande zote.

Bunge la Kenya limeidhinisha kuondolewa kwa Naibu wa Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua katika nafasi hiyo baada ya Wabunge 281 kati ya 325 kupiga kura ya kusema aondoke kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kujitajirisha na kuibua chuki za kikabila.

Kiwango kilichowekwa na katiba ni angalau wabunge 233.

DKT NCHIMBI AIGEUKIA WIZARA YA KILIMO | ATAKA MBEGU ZENYE UBORA ZIFIKE KWA WAKULIMA HARAKA

Leave a Comment