
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Zuhura Yunus mapema Leo, Oktoba 9, ametembelea eneo la uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya maandalizi ya maadhimisho ya kilele cha Mwenge wa Uhuru kinachotarajiwa kufanyika, Oktoba 14,2024. Wakati akikagua uwanja huo, Zuhura Yunus aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda