×

Chadema: Sio Kila Mradi Wa Serikali Unapaswa Kupingwa – Video

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema.

Viongozi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamepongeza utekelezaji wa mradi wa Treni ya mwendokasi SGR na wameeleza kuwa sio kila mradi wa serikali unapaswa kupingwa, bali kuungwa mkono kwani unaleta manufaa kwa wananchi.

Hayo yamejiri baada ya viongozi hao Viongozi hao, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, pamoja na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema, kutumia usafiri wa Treni hiyo kwa mara ya kwanza wakati wa safari yao kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma mnamo Oktoba 10, 2024.

Aidha, wametoa maoni kuhusu filamu ya Royal Tour inayooneshwa ndani ya treni hiyo na kusema kuwa hatua hiyo ni ya kipekee katika kuhamasisha utalii.

KWA MARA ya KWANZA CHADEMA WAPANDA SGR – WAFUNGUKA – “SIYO KILA MRADI wa SERIKALI UNAPASWA KUPINGWA”

Leave a Comment