Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku mashabiki kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mechi ya Simba na Yanga wakiwa na silaha ya aina yoyote.
Kamanda wa Polisi, SACP Jumanne Muliro amesema watakaoruhusiwa kuingia na silaha ni askari wachache watakaopangiwa kazi maalum za kiusalama kwenye uwanja huo.