
Watu 14 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo, katika daraja la Kikafu, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Akitoa taarifa ya ajali hiyo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu za usiku, baada ya Lori na basi dogo la kubeba abiria (Coaster) iliyokua ikigokea Moshi kuelekea Arusha, kugongana katikati ya daraja hilo.

Amesema watu sita walifariki palepale na wenginr nane (8) walifariki wakiwa wanakimbizwa hospitali.
Majeruhi wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kcmc,Mawenzi na hospitali ya Hai.