
WABUNGE wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee pamoja na swahiba wake, Esther Matiko wamefika katika Viwanja vya Magufuli kuungana na familia, viongozi, wananchi na waombolezaji wengine katika ibada ya maziko ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa, Machi 26, 2021.