The House of Favourite Newspapers

Ajib: Imebaki Yanga tu! Tunaisubiri

0

Ajib-mpiraMshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
WAKATI Simba ikitarajiwa kukipiga na Stand United kesho Jumamosi mkoani Shinyanga, mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amesema kuwa mechi ngumu iliyobaki kwao ni Yanga kutokana na wachezaji wa timu zote kukamiana.
Februari 20, mwaka huu, Simba na Yanga zitakutana katika mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba itakuwa chini ya Kocha Jackson Mayanja ambaye ameiongoza  timu hiyo kushinda mechi sita mfululizo.
Ajib amekuwa katika kiwango cha juu kwa hivi sasa huku akiwa ameshafunga mabao nane katika ligi kuu, hivyo anaweza kuwa mchezaji muhimu katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ajib alisema wanachokiangalia ni ushindi tu katika kila mechi iliyopo mbele yao lakini anaamini mechi yao dhidi Yanga itakuwa ngumu tofauti na watu wanavyofikiria.
“Yanga ni timu nzuri kutokana na aina ya wachezaji wao, imebakia mechi hiyo ambayo naamini itakuwa ngumu sana kwa sababu kila timu itakuwa inahitaji matokeo ya ushindi  lakini timu yetu ipo vizuri na hatuwezi kuwahofia kwa sababu malengo yetu ni kushinda kila mchezo.
“Waje tu, kazi itaonekana kati yetu nani anastahili ushindi, ingawa dakika 90 ndizo zitatoa majibu ya kweli, tusubiri tuone itakuwaje,” alisema Ajib.

Leave A Reply