×

Polisi Kuwakamata Waliokuwa Wakijaribu Kumkamata Deogratius Tarimo, Pwani

Jeshi la Polisi kupitia Msemaji wake, David A. Misime – DCP linachunguza picha mjongeo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha watu ambao wanajaribu kumkamata na kujaribu kumwingiza kwa nguvu ndani ya gari Bw. Deogratius Tarimo ambaye ni Mfanyabiashara na Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani. Tukio hili liliripotiwa na yeye mwenyewe katika kituo cha Polisi Gogoni Jijini Dar es Salaam Novemba 11, 2024.

Kulingana na ushahidi uliowasilishwa kituoni hapo na yeye mwenyewe ni kwamba, chanzo cha tukio na kilichomsukuma kufika katika Hoteli ya Rovenpic iliyopo eneo la Kiluvya Jijini Dar es Salaan ni kufanya mazungumzo ya biashara ambayo amekuwa akiwasiliana kuifanya na aliokuwa anawasiliana nao toka Oktoba 25, 2024.

Jeshi la Polisi linahakikisha litawakamata watu waliokuwa wakijaribu kumkamata na kujaribu kumwingiza kwenye gari kama inavyoonekana katika picha mjongeo huo kulingana na ushahidi ambao umeshakusanywa na unaoendelea kukusanywa ili hatua zingine ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria kwani hakuna aliye juu ya sheria.

KIMENUKA MWANZA: WEZI wa NYAVU za UVUVI WASAKWA KILA KONA ZIWA VICTORIA….

Leave a Comment