
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Msigwa pia ameongezewa jukumu la Usemaji Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Thobias Makoba allyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.
