×

Wafanyakazi jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere wagoma

1.Wafanyakazi hao wakishikilia mabango yenye ujumbe. Wafanyakazi wa jengo hilo wakishikilia mabango yenye ujumbe.
3.Mabango yaliyoandikwa ujumbe yakitawala eneo hilo.Mabango yaliyoandikwa ujumbe yakitawala eneo hilo.
4..Jengo linalojengwa eneo la Barabara ya Kilwa maeneo ya Bandari jijini Dar.Jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere linalojengwa.
5.Taswira ya nje ya jengo hilo.Taswira ya nje ya jengo hilo.

WAFANYAKAZI wa Kitanzania wanaojenga jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kampuni ya Kichina ya CRJE lililopo Barabara ya Kilwa maeneo ya bandari walijazana leo nje ya jengo hilo jijini Dar es Salaam kwa madai kushinikiza kupewa mikataba.

Mtandao huu ulipita maeneo hayo na kuwakuta wafanyakazi wa ujenzi wa jengo hilo wakiwa nje na mabango na kufanikiwa kunasa picha zinazoonesha tukio husika.

Mmoja wa wafanyakazi wa jengo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Kasikasi Adam alipohojiwa na mwandishi wetu kisa cha kukaa nje kugoma badala ya kuwa ndani wakifanya kazi alisema kuwa wameamua kugoma wakishinikiza kupewa mikataba ya kudumu. Aidha alisema sababu nyingine ni malipo wanayolipwa kwa siku ambayo ni kiasi cha sh. 6.000 kuwa hakitoshi, hatua ambayo iliwafanya kugoma.

Mwandishi wetu alipoingia ndani ya uzio unaozunguka ujenzi huo ili aweze kuonana na uongozi kuzungumzia sakata hilo hakupatikana msemaji yeyote bali walikutwa walinzi ambao walidai kuwa msemaji hawajui alipokwenda.

(Na Denis Mtima/Gpl)

Leave a Comment