×

Dua ya Kuliombea Taifa Yafanyika Mkuranga na Kuhudhuriwa na Mawaziri, Viongozi wa Dini

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ameungana na wananchi wa wilaya hiyo, kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake na kuliombea Taifa ili liwe na amani, umoja na mshikamano utakaowezesha maendeleo endelevu.

Dua hiyo imefanyika Jumamosi ya Desemba 14, 2024 katika Uwanja wa Shule Msingi Mkuranga mkoani Pwani ambapo ilihudhuriwa na viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri, wabunge na maelfu ya wananchi kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo.

Dua hiyo ilitanguliwa na Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika asubuhi yaliyowakutanisha masheikh mbalimbali waandamizi wakiwemo wa mikoa ya Arusha, Kigoma, Kagera, Dar es Salaam na Pwani.
Katika dua hiyo ujumbe mkubwa uliotawala ni amani ambapo Watanzania wamesisitiziwa kuitunza ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia ambaye kwa nyakati tofauti amekuwa mstari wa mbele kuhubiri amani.

Mbali hilo, suala la maadili lilisisitizwa kwa kiwango kikubwa kwa kuelezwa kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anatunza na kuyalinda maadili kwa manufaa ya Taifa.

 

Leave a Comment