×

Shigongo: Magufuli Alijitoa Sadaka Maisha, Uhai Wake – Video

 

MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo, ameeleza maazimio yake kama mbunge na mwananchi wa Taifa hili katika kuenzi utendaji wa Hayati Magufuli pamoja na kumpongeza Rais Samia.

 

“Nina kila sababu ya kujivunia kuwa na Kiongozi kama Magufuli, alijitoa sadaka maisha yake na uhai wake kwa ajili ya Watanzania maskini, ameuthibitishia ulimwengu kuwa Tanzania inaweza kuendesha mambo yake bila kumtegemea mzungu. Tulaiminishwa kwamba hatuwezi kufanya lolote bila wazungu. Magufuli ametuthibitishia Watanzania kuwa Tanzania ni tajiri, na mimi leo nasema ninatoka Tanzania Taifa tajiri.

 

“Nchi yetu leo ipo uchumi wa kati, zipo nchi ziliingia uchumi wa kati zinarudi nyuma, sisi tunao wajibu wa kujituma kwa nguvu na kuteseka kutimiza ndoto za Mhe Rais wetu ambaye ametangulia mbele za haki.

 

 

“Najaribu kuwaza wakati Mhe. Magufuli anaondoka alikuwa akiwaza nini, alitamani kuona mabasi yakipita juu ya daraja la Busisi, alitamani kuona treni ikipita kwa kasi pale Tazara. Kazi yetu ni kumpa silaha kwa kuyatimiza yale aliyoanzisha.

 

“Moyonmo mwangu sina wasiwasi na Mhe Rais Mama Samia, wanawake wana uwezo mkubwa sana. Nina uhakika nchi yangu iko mikono salama na atalivusha Taifa hili kwenda uchumi wa juu zaidi. Mhe. Mpango tunaamini atamsaidia Rais wetu kuipeleka nchi yetu pazuri, sisi tunao wajibu wa kumuunga mkono ili kutimiza yale aliyokusudia kulifanyia Taifa letu,” – Eric Shigongo, Mbunge wa Buchosa.

 

Leave a Comment