×

Mshambuliaji Lookman Ashinda Ballon d’or ya Afrika, Washindi Wapo Hapa

Mshambuliaji wa klabu ya Atalanta ya Italia na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman

Mshambuliaji wa klabu ya Atalanta ya Italia na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la soka Afrika (Ballon d’or) kwenye tuzo za CAF zilizofanyika Mjini Marrakesh , Morocco.

Lookman (27) amewashinda Simon Adingra wa Ivory Coast, Serhou Guirassy wa Guinea, Achraf Hakimi wa Morocco na Ronwen Williams wa Afrika Kusini.

2. Kiungo mshambuliaji wa klabu ya AS Monaco na timu ya taifa ya Senegal, Lamine Camara ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa mwaka wa Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa wanaume akiwashinda Karim Konate na Oumar Diakite.

3. Kwa upande wa wanawake, tuzo ya mchezaji bora chipukizi imekwenda kwa Doha El Madani kutoka Morocco

4. Nyanda wa klabu ya Mamelodi Sundowns na Timu ya taifa ya Afrika Kusini, Ronwen Williams ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika wa mwaka 2024 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani.

5. Klabu ya Al Ahly ya Misri na Mabingwa wa Afrika 2024 imeshinda tuzo ya timu ya mwaka 2024 kwa ngazi ya klabu ikifanya hivyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

6. Kwa upande wa Wanawake tuzo hiyo imekwenda kwa timu ya wanawake ya TP Mazembe.

7. Timu bora ya mwaka kwa ngazi ya kimataifa kwa wanaume ni Ivory Coast huku Nigeria ikishinda tuzo hiyo kwa upande wa Wanawake.

8. Kocha wa timu ya Taifa ya lvory Coast, Emerse Fae ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2024 wa Afrika akiwashinda kocha wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Hugo Broos na kocha wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sebastien Desabre.

9. Kikosi bora cha Mwaka 2024 Afrika kwa Wanaume, Ronwen Williams ametemwa huku Andre Onana wa Manchester United akijumuishwa sambamba na Mohammed Kudus, Ademola Lookman na Mohammed Salah.

10. Kiungo wa Timu ya Wanawake ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Barbra Banda raia wa Zambia ameshinda Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2024 kwa upande wa Wanawake.

11. Kikosi bora cha Mwaka 2024 Afrika kwa Wanaume, Ronwen Williams ametemwa huku Andre Onana wa Manchester United akijumuishwa sambamba na Mohammed Kudus, Ademola Lookman na Mohammed Salah.

KIKOSI BORA CHA MWAKA CAF
🇨🇲 André Onana
🇲🇦 Achraf Hakimi
🇸🇳 Kalidou Koulibaly
🇨🇩 Chancel Mbemba
🇲🇦 Sofyan Amrabat
🇨🇮 Franck Kessié
🇲🇱 Yves Bissouma
🇬🇭 Mohammed Kudus
🇪🇬 Mohamed Salah
🇳🇬 Victor Osimhen
🇳🇬 Ademola Lookman

WATU TISA WAKAMATWA kwa KOSA la KUTAKA KUOZESHA MWANAFUNZI – KAMANDA ATOA TAMKO ZITO…

Leave a Comment