×

Video: Mama Wa Miaka Afariki Baada Ya Kung’atwa Na Nyoka, Uzembe Wahusishwa


Juliana Obed, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 kutoka Kijiji cha Magugu wilayani Babati mkoani Manyara, amefariki dunia baada ya kuumwa na nyoka.

Tukio hilo limetokea mnamo Desemba 15, 2024 majira ya saa 11 jioni wakati alipokuwa akichuma mboga nje ya jengo la Kanisa la Magugu, ambalo mume wake alikuwa akilipaua.

Kwa mujibu wa mume wa marehemu, Obed Laizer, baada ya tukio hilo alimkimbiza mke wake katika Kituo cha Afya cha Magugu kwa ajili ya matibabu.

Leave a Comment