
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia ameunda Tume ya Rais ya Kutathmini kuhusu Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro ambapo amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Gerald Ndika kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kufanya tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Eneo la Hifadhi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unakuja baada ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kukutana na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai wanaoishi eneo la Hifadhi la Ngorongoro mnamo Desemba 01, 2024 ambapo alitangaza uamuzi wa Serikali kuunda Tume mbili.
Tume ya Kwanza itafanya tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Tume ya Pili itaangalia utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kutoka eneo la Hifadhi hiyo.
Dkt. Samia amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Tume ya kwanza:-
(i) Bw. Philemon Luhanjo – Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu;
(ii) Bi. Zakia Hamdani Meghji – Aliwahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii;
(iii) Jaji George Mcheche Masaju – Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria;
(iv) Dkt. Richard Muyungi – Mshauri wa Rais, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi;
(v) Balozi Salome Sijaona – Balozi na Katibu Mkuu Mstaafu;
(vi) Prof. Wilbard Kombe – Profesa wa Chuo Kikuu Ardhi;
(vii) Prof. Emmanuel Luoga – Profesa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo;
(viii) Bw. Mollel James Moringe – Diwani na Katibu wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro;
(ix) Bi. Moi Aprakwa Sikorei – Diwani na Mkazi wa Ngorongoro.
Kwa upande wa Tume ya pili, Rais Dkt. Samia amemteua Mhandisi Musa Iyombe, Katibu Mkuu Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo ambapo wajumbe walioteuliwa ni:-
(i) Bi. Sihaba Nkinga – Katibu Mkuu Mstaafu;
(ii) Bw. Alphayo Kidata – Mshauri wa Rais, Uwezeshaji Biashara na Masuala ya Kodi;
(iii) Balozi Valentino Mlowola – Balozi Mstaafu na aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU);
(iv) Balozi Mohamed Mtonga – Balozi mstaafu na aliwahi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali;
